Ujumbe mfupi toka kwa Mwenyekiti wa IJAWOSA LTD
Awali ya yote nashukuru Mungu kwa kutupa kibali cha kuendelea kutekeleza majukumu yetu ya kila siku na kwa umoja wetu, nashukuru Bodi, Kamati ya Usimamizi na Kamati ya Mikopo, Watendaji wa Chama na Wanachama wote. IJAWOSA LTD ni Chama ambacho misingi yake imejengwa ndani ya Ushirika, kinachoendesha majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya Ushirika nchini Tanzania.
Kwa niaba ya IJAWOSA LTD napenda kuwaalika Watumishi wa Serikali katika Mkoa wa Tanga, Mikoa jirani, hususani Wilaya yetu yetu ya Lushoto.
Kupitia IJAWOSA LTD utakuwa na furaha wakati wote wa Utumishi wako kwa vile masuala yote yahusuyo fedha kama vile kuanzisha ama uwekezaji mdogo mdogo wa biashara, ada za watoto, akiba na maendeleo yako, utawezeshwa na Chama kwa kuwekeza Akiba kidogo kidogo. Pia utapata Elimu kabla ya kukopa, jambo ambalo ni muhimu mno.
IJAWOSA LTD inaamini kuwa ” Ukitaka kufika haraka nenda peke yako, bali ukitaka kufika mbali nenda na wenzako” kwa umoja wetu hakika tutafika mbali kwa pamoja na kwa uhakika.
Tayari IJAWOSA LTD imefungua milango kwa Wafanyakazi wote wa Halmashauri ya Wilaya Lushoto kujiunga na tayari tumesaini fungamano la ushirikiano (MoU).
Nichukue fursa hii kuwaalika Wafanyakazi wa wa Serikali kutoka Taasisi mbalimbali kujiunga na IJAWOSA LTD kwa kupitia nyaraka mbalimbali zilizopo katika Tovuti hii kama Masharti ya Chama, Miongozo na kisha kujaza fomu yako kidigitali, itapokelewa na kufanyiwa kazi.
Pamoja na Salamu za Chama.