TAARIFA FUPI YA CHAMA
Slogan ya Chama = IJAWOSA – CHAMA CHANGU MTAJI WANGU
A: UTANGULIZI
IJA WORKERS SACCOS LTD (IJAWOSA LTD) ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo. kilianzishwa mwaka 2010 na Wafanyakazi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA-LUSHOTO). Chama kilisajiliwa mwaka 2010 na kupewa Hati Namba.TAR 526 na kupata Leseni Daraja A kwa mujibu wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 mwaka 2021.
Mwaka 2022 Wanachama kupitia Mkutano Mkuu wa kawaida walifungua fungamano la Pamoja na kuwa *WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA, MATAWI YAKE AU WAJIRIWA WA SERIKALI KATIKA WILAYA YA LUSHOTO PAMOJA NA WAAJIRIWA WA IJA WORKERS SACCOS LIMITED*
B: DIRA YA IJAWOSA
Kuwa SACCOIS bora yenye kuinua uchumi kwa Wanachama wake.
C: DHIMA YA CHAMA
Kuwa SACCOS inayojitegemea na kutoa huduma stahiki kwa tija na ufanisi.
D: MAONO YA CHAMA
Kuwa SACCOS inayojitegemea na kutoa huduma stahiki kwa tija na ufanisi.
F: MUUNDO WA CHAMA
- Bodi ya Chama
Chama kina wajumbe wa Bodi watano (5) ambao ni:-
Mwenyekiti
Makamu Mwenyekiti na
Wajumbe watatu (3)
- Kamati ya Usimamzi
Kamati hii inaundwa na wajumbe watatu(3) ambao ni:-
Mwenyekiti
Na wajumbe wawili (2)
- Kamati ya Mikopo
Kamati hii inaundwa na wajumbe watatu (3) ambao ni:-
Katibu
Wajumbe wawili (2)
Wajumbe wa Kamati hii wanatoka katika Bodi ya Chama
- Watendaji
Chama kina Watendaji wanne (4) ambao ni
Meneja
Mkaguzi wa ndani
Afisa Mikopo na
Karani
G: HUDUMA ZITOLEWAZO NA CHAMA
1.Mikopo ya aina mbalimbali
- Mikopo ya Maendeleo – miaka 2 had 5 riba 11%
- Mikopo ya Dharura – mwaka 1 riba 10%
- Mikopo ya Elimu – mwaka 1 riba 5%
- Mikopo ya Chap Chap/Safari – miezi 3 riba 10%
2.Huduma za Uwakala wa Fedha
- FAHARI HUDUMA
- NMB WAKALA
- M-PESA
- AIRTEL MONEY
- HALOPESA
H: MAFANIKIO YA CHAMA
- Kulipa riba juu ya akiba kwa asilimia 3% kila mwaka
- Kuwa na huduma nafuu na bora kwa wanachama wake
- Kulipa Gawio kwa wanachama wake pale inapotokea faida
- Kutoa mikopo kwa haraka ndani ya masaa yasiyozidi 24.
I: MAONO YA CHAMA
- Kuimarisha hali ya Uchumi wa wanachama wake kwa kuwapa mikopo yenye gharama nafuu, elimu ya mikopo na kuwapa huduma jumuishi za kifedha;
- Kukuza Chama kutoka Daraja A kwenda Daraja B kwa kuongeza idadi ya wanachama kutoka 70 waliopo sasa hadi 150 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kukuza mtaji kwa kuwa na miradi mbalimbali ya maendeleo kwa chama na mwanachama mmoja mmoja ili kutekeleza jambo hili tayari Chama kimesaini Fungamano la Ushirikiano kati ya IJAWOSA LTD na Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto (MoU) ili kutanua wigo wa kupata wanachama wapya na kukuza mtaji;
- Kufikia uwezo wa kujitegemea na kuwa na ofisi ya Chama.
J: NAMNA YA KUJIUNGA NA IJAWOSA.
i .Tuma maombi ya barua ya kujiunga na Chama kwa Mwenyekiti IJAWOSA ama jaza fomu ya kujiunga;
ii.Kulipa kiingilio shilingi elfu kumi tu (10,000/=);
iii.Barua kwa muajiri kwajili ya michango ya Akiba ya kila mwezi.
K: MWANACHAMA KAMILI WA IJAWOSA
- Awe Mtumishi wa Serikali;
- Awe na uwezo wa kuweka Akiba Tshs.50,000/=au zaidi kila mwezi kutoka katika Mshahara wake
- Awe anamiliki Hisa kumi (10) ambayo kila Hisa inathamani ya Tshs.50,000/sawa na jumla ya Tshs.500,000/
- Awe amejaza fomu ya kujiunga kwa usahihi na makato yake kuthibitishwa na Afisa utumishi ama Mwajir wake.
- Siku tisini baada ya kujiunga rasmi,atakuwa na uwezo wakuomba Mikopo.