IJA WORKERS SACCOS LTD (IJAWOSA LTD)

IJA WORKERS SACCOS LTD (IJAWOSA LTD) ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo. kilianzishwa mwaka 2010 na Wafanyakazi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA-LUSHOTO). Chama kilisajiliwa mwaka 2010 na kupewa Hati Namba.TAR 526 na kupata Leseni Daraja A kwa mujibu  wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 mwaka 2021.

Mwaka 2022 Wanachama kupitia Mkutano Mkuu wa kawaida walifungua fungamano la Pamoja na kuwa *WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA, MATAWI YAKE AU WAJIRIWA WA SERIKALI KATIKA WILAYA YA LUSHOTO PAMOJA NA WAAJIRIWA WA IJA WORKERS SACCOS LIMITED

 SACCOIS bora yenye kuinua uchumi kwa Wanachama wake.

SACCOS inayojitegemea na kutoa huduma stahiki kwa tija na ufanisi.

MAONO YA CHAMA

  • Kuimarisha hali ya Uchumi wa wanachama wake kwa kuwapa mikopo yenye gharama nafuu, elimu ya mikopo na kuwapa huduma jumuishi za kifedha;
  • Kukuza Chama kutoka Daraja A kwenda Daraja B kwa kuongeza idadi ya wanachama kutoka 70 waliopo sasa hadi 150 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kukuza mtaji kwa kuwa na miradi mbalimbali ya maendeleo kwa chama na mwanachama mmoja mmoja ili kutekeleza jambo hili tayari Chama kimesaini Fungamano la Ushirikiano kati ya IJAWOSA LTD na Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto (MoU) ili kutanua wigo wa kupata wanachama wapya na kukuza mtaji;
  • Kufikia uwezo wa kujitegemea na kuwa na ofisi ya Chama.

.